Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Mhando |
TANGANYIKA
Mkuu wa wilaya ya
Tanganyika Mkoani Katavi Salehe
Mhando ameiagiza kukamatwa kwa watu walio wazuia wananchi 160 katika kijiji cha Kaseganyama kata ya
Kasekese kufanya shughuli za kilimo
kwenye maeneo halali.
Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho Mhando amesema serikali ya kijiji hicho kwa kushilikiana na serikali ya wilaya kwa pamoja waliamua kutenga hekari 1280 baada ya wananchi hao kukubali kuondoka katika maeneo ya hifadhi jambo ambalo halijafanikiwa kutokana na vitisho wa kikundi hicho.
Aidha katika kukabiliana na uhalifu ametoa siku kumi na nne kwa watu wanaomiliki
silaha kinyume na sheria kuzisalimisha katika ofisi za watendaji na vituo vya
polisi vya wilaya hiyo kabla ya msako kuanza.
Katika zaiara hiyo pia
amekagua na kushiliki na wanachi katika shughuli za ujenzi wa shule ya
sekondari Simbwesa na shule ya sekondari Kasekese ambazo zipo katika hatua ya
lenta.
Chanzo: Paul Matius
No comments:
Post a Comment