TABORA
Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoa wa Tabora, Angelina
Kwingwa ametangaza kuwachukulia hatua sambamba na kuwafilisi viongozi wa vyama
vya msingi wanaotuhumiwa kuwadhulumu wakulima fedha za mauzo ya Tumbaku.
DC Kwingwa ameyasema hayo katika mkutano wa
viongozi wa vyama vya msingi na wakulima wa wilaya ya Urambo.
Amesema viongozi hao wamekuwa wakilalamikiwa na
wakulima kwa kutokuwa waadilifu, na kwamba endapo watabainika kuwadhulumu
wakulima watafilisiwa ili kufidiwa fedha za wakulima.
Katika hatua
nyingine, Kwingwa amewataka wakulima wilayani humo kuboresha zao la tumbaku kwa
kupanda miti kwa ajili ya kukaushia zao hilo.
Chanzo: Mo blog
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment