Monday, 5 February 2018

MWANASIASA mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru anatarajiwa kuzikwa leo saa tisa alasiri.

Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru enzi za uhai wake

Dar es Salaam.
MWANASIASA mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru anatarajiwa kuzikwa leo saa tisa alasiri katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya maziko ya mwanasiasa huyo, Omary Kimbau inaonesha kuwa jana saa 10 jioni mwili wa marehemu ulitolewa Hospitali ya Muhimbili na kupelekwa nyumbani kwake Victoria/Makumbusho ambako ibada ilifanyika kisha kufuatiwa na mkesha.
Hata hivyo leo, shughuli zitakazofanywa ni kama ifuatavyo: saa 1:00 asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi. Saa 4:00 asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani kwa marehemu, Saa 6:00 mchana 9:00 kuaga mwili wa marehemu kwenye Ukumbi wa Karimjee.
Kingunge alifariki dunia Ijumaa alfajiri wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alipokuwa akiuguza majeraha baada ya kung’atwa na mbwa mwishoni mwa mwaka jana nyumbani kwake.


Enock Mwiru ambaye ni mdogo wa marehemu alisema kuwa wamepata pigo kubwa kwani Kingunge alikuwa ni kiunganishi cha familia.
Chanzo:habari leo
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...