NSIMBO
Kituo cha kulea watoto
wanaoishi katika mazingira magumu na yatima Gethseman kilichopo kata ya
litapunga halmashauri ya Nsimbo mkoani katavi kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo uchakavu wa mabweni.
Hayo yamesemwa na
Katibu wa kituo hicho Bruda Samweli Edward Lumanyika wakati akizungumza na wafanyakazi
wa mpanda radio katika kituo hicho wakati walipotembelea kituoni hapo kwa ajili
ya kupeleka msaada kwa watoto wa kituo hicho.
Aidha bruda samweli
amesema kituo kimekua kikisaidia serikali kuhifadhi watoto ambao wanakabiliwa
na matatizo ya unyanyasaji wa kijinsia na kuiomba serikali kuona umuhimu wa
kusaidia kituo hicho ili kuweza kuwasaidia katika kutimiza malengo ya watoto
hao.
Kwa upande wao watoto
wa kituo hicho wameishukuru mpanda radio kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia na
kuiomba jamii kujitokeza na kusaidia changamoto zinazowakabili.
Kituo cha Gestheman
kilianzishwa mwaka 1993 kikiwa na lengo la kulea watoto yatima pamoja na watoto wanaolelewa katika mazingira
magumu kwa kutegemea kilimo.
CHANZO:RESTUTA NYONDO
No comments:
Post a Comment