kiongozi wa upinznai nchini Kenya Raila Odinga
WASHNGTON
Serikali ya Marekani imesema imesikitishwa na hatua
ya kiongozi wa upinznai nchini Kenya Raila Odinga ya kujiapisha Jumanne wiki
hii.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema taifa
hilo linaamini mizozo yoyote ile inafaa kutatuliwa kwa njia zifaazo kisheria.
Bw Odinga alisusia uchaguzi huo wa marudio na
amesema hamtambui Rais Kenyatta kama rais halali wa taifa hilo.
Mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, ambaye ni
makamu wa rais wa zamani, hakuhudhuria sherehe hiyo ingawa walikuwa wameahidi
kuapishwa wote wawili kwa pamoja.
Chanzo:Bbc swahili
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment