Thursday, 1 February 2018

Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani katavi ni kikwazo cha utengenezaji wa barabara katika baadhi ya maeneo ya Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.


MPANDA

Mvua zinazoendelea kunyesha  mkoani katavi ni kikwazo cha utengenezaji wa barabara  katika baadhi ya maeneo ya  Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.

Hayo yamebainishwa na meneja wa tarura manispaa ya mpanda mhandisi  kyado wakati akizungumza na mpanda radio ambapo amesema kuwa wanashindwa kusambaza vifusi kwasababu ya mvua zinazoendelea kunyesha .

Zuberi  kiwenge mratibu wa Tarura mkoa wa katavi amesema wananchi  wana haki ya kufika katika ofisi zao na kuhoji kinachioendelea juu ya utengenezaji wa barabara lakini si madiwani kwani kwa sasa hawako chini yao.

Tarula  ambao ni wakala wa utengenezaji wa barabara mijini na vijini hapo awali  walikua chini ya halmashauri lakini kwa sasa ni tasisi inayojitegemea katika utendaji kazi.


Source ester

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...