NSIMBO
Kucheleweshwa kwa pembejeo za zao la tumbaku kumetajwa kuwa chanzo cha
kushuka kwa zao hilo katika wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi.
Hayo yamebainishwa katika kikao maalumu cha baraza la madiwani katika
halmashauri ya wilaya ya Nsimbo kilichofanyika leo na ambapo mkuu wa idara ya
kilimo,umwagiliaji na ushirika George Magile katika wilaya hiyo amesema
pembejeo zimekuwa hazifiki kwa wakati hali inayosababisha wakulima kushindwa
kulima zao hilo kwa muda unaotakiwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza hilo Raphael Kalinga amewaomba
madiwani na viongozi wa idara kusimamia mazao mbadala kama korosho na alizeti
ili yaweze kuinua uchumi wa wananchi.
Zao la tumbaku ni miongoni mwa mazao ya biashara yanayolimwa katika
mkoa wa katavi .
No comments:
Post a Comment