MPANDA
Wananchi wanaoishi katika mtaa
wa tambuka reli kata ya mpanda hotel
manispaa ya mpnda mkoani katavi wameiomba serikali kuwaongezea muda wa
kuhamisha makazi yao katika maeneo hayo.
Wamesema hayo wakati
wakizungumza na mpanda radio na kuiomba serikali kuwa saidia kuwaongezea muda
ili waweze kupata maeneo mengine ya kuishi kutokana na serikali kuwahamisha
bila kuwapatia maeneo mengine ya kujiendeleza kimaisha
Aidha wakazi hao wamesema
kuwa hakuna tamko lolote lile lililotolewa na serikali kuhusu maeneo
wanayotakiwa kuishi hali inayopelekea kubaki na sintofahamu.
Serikali ilitoa maagizo kwa
wanchi hao kuhama tangu mwaka jana ambapo iliwataka mpaka kufikia January
mwaka2018 wandoke na kupisha shughuli za kiserekali kuendeelea katika maeneo hayo.
Chanzo:Issack Gerald
No comments:
Post a Comment