MPANDA
Wakulima
wa Tumbaku Mkoani Katavi wanakabiliwa ugumu wa maisha
kutokana na ucheleweshaji wa masoko ya
ununuzi wa Zao hilo katika maeneo yao.
Wakizungumza
na mpanda redio kwa nyakati tofauti katika ofisi za godauni ya TLTC Mpanda mjini wamesama kutokana na kucheleweshwa kwa masoko
inaawawia vigumu kufanya shughuli za maendeleo kutokana na kutegemea fadha ya
tumbaku katika kuendesha maisha yao ya kila siku
Aidha
wamesema licha ya serikali kutoa siku saba kwa vyama vya msingi kuwalipa malipo
yao ya tumbaku bado malipo hayo hayajafanyika kama serikali ilivyoagiza hali
ambayo inaendelea kufanya maisha yao yawe ghari kutokana na ucheleweshwji wa
malipo hayo
Kwa
upande wake meneja wa masoko na
usafirishaji wa kampuni ya TLTC Mkoa wa
katavi bwana Onesmo Aloyce Kiwesi amesema zoezi la kununua Tumbaku ambayo
ilikuwa ndani ya mkataba na wakulima walimaliza
kwa wakati na zoezi linalo endelea sasahivi ni kununua Tumbaku ambayo ilizidi
kwa wakulimaAmbayo ipo nje ya mkataba na
wanatarajia kumaliza zoezi hilo mnamo tarehe 20 /2/2018.
Chanzo:Paul Mathias
No comments:
Post a Comment