Wakazi wa Mtaa wa Mpadeko kata ya Mpanda hoteli iliyopo halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda wamelalamikia uchafuzi wa mazingira unaotokana na viwanda
vya karanga.
Wameyasema hayokwa nyakati tofauti
walipozungumza na Mpanda radio wameitaka serikali kubadili eneo la
uendeshwaji wa viwanda ili kuepusha madhara yanayo weza kujitokeza kiafya
kufuatia vumbi kali wakati viwanda hivyo vikifanya kazi .
Kwa upande wake mmoja wa wamiliki wa viwanda hivyo amesema wanasubiri
serikali kuwaonyesha maeneo mbadala yatakayo kuwa nje ya makazi ya watu.
Uwekezaji unaohimizwa sasa kwa kasi lazima uzingatie mahitaji ya sheria
mbalimbali zilizopo kama Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004, na Sheria ya
Mipango miji ya mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment