Baadhi ya waendesha
Bodaboda Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamekuwa wakiwalalamikia askali wa
usalama barabarani kukamata pikipiki zao bila makosa.
Wakizungumza na Mpanda
Radio wamebainasha kwa mara kadhaa piki
piki huchukuliwa kinguvu wakati mwingine zikiwa zimeegeshwa bila taarifa kwa
mhusika.
Mkuu wa usalama
barabarani Mkoa wa Katavi Wille Joasi
Mwamasika amekanusha taarifa hizo akidai kuwa
kufanya hivyo ni kinyume cha sheria katika utendaji kazi wa kitengo cha
usalama barabarani.
Idadi ya vijana wanao
jiajiri kupitia udereva piki piki maarufu kama boda boda imekuwa ikiongezeka
kila mwaka lakini ikikabiliwa na vikwazo lukuki kutoka taasisi mbali mbali za
Serikali.
No comments:
Post a Comment