Mganga Mkuu mkoani Katavi Dr Omary Sukari
Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kuchukua tahadhari
dhidi ya ugonjwa hatari wa ebola
Mganga mkuu wa mkoa wa katavi DK Omary Sukari
ameimbia Mpanda radio kuwa kuna mikakati kadhaa ambayo wameiweka baada ya
kupata taarifa za tishio la kuwepo kwa ugonjwa wa ebola katika nchi ya Kongo.
Dk Sukari amesema tayari wameshatoa elimu kwa njia
ya vipeperushi katika eneo la Karema linalopakana na nchi ya Congo ambayo ni
chimbuko la ugonjwa huo
Ugonjwa wa ebola uligundulika mwaka 1976 ambapo hadi
kufikia mwaka 2014 takribani watu 1740 walipata maambukizi katika nchi za
Afrika magharibi ikiwemo Liberia, Sierra Lione na Nigeria
Chanzo: Ester Baraka
No comments:
Post a Comment