Waendesha pikipiki
maarufu kama bodaboda wameiomba serikali kutoa elimu kwa wananchi juu ya uvaaji
wa kofia ngumu pindi wanapotumia usafiri huo ili kujikinga na ajali za
barabarani.
Wakizungumza na Mpanda
redio kwa nyakati tofauti ambapo ni takribani wiki moja kupita baada ya agizo
la kila dereva wa pikipiki kuwa na kofia mbili ili aweze kufanya kazi hiyo bila
kufuatiliwa na askari wa usalama barabarani
Aidha wamesema abiria
wanawakwamisha kwa kukataa kuvaa kofi hizo kwa kisingizo cha kuogopa
kuambukizwa magonjwa kutokana na kutumiwa na watu wengi.
Hivi karibuni jeshi la polisi kitengo cha usalama
barabarani mkoa wa Katavi lilitoa siku saba kwa kila dereva boda boda kuwa na
kofia ngumu mbili.
Chanzo:Rebacca
kija
No comments:
Post a Comment