Shirika la umeme Tanzania Tanesco
Mkoani katavi limesema liko katika mipango ya mwisho katika ukamilishaji wa
usambazaji wa umeme wa Rea awamu ya tatu
Katika mpango huo ambao umetajwa
kuvifikia vijiji 117 unatarajiwa kuanza mara moja tu baada ya mkandarasi
kupatikana
Akizungumza na Mpanda radio kwa njia
ya simu Meneja Uhusiano na wateja Amon Maiko amebainisha kuwa kukamilika kwa
mpango huo kutapunguza kero ya upatikanaji wa umeme katika baadhi ya maeneo
mkoani hapa.
Hivi karibuni Waziri wa Nishati,
Dkt. Medard Kalemani amewaagiza Watendaji wa TANESCO Nyanda za Juu Kusini
Magharibi, Wizara ya Nishati, na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kabla ya Juni
mwaka 2021 kuhakikisha kuwa zaidi ya asilimia 85 ya wananchi wawe
wameunganishwa na huduma ya umeme kufikia mwaka huo.
Chanzo:Ezelina Yuda
No comments:
Post a Comment