Wafanyabiashara
wa stendi ya mabasi yaendayo mikoani katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
Mkoani Katavi wameiomba serikali kupunguza tozo za taka kutokana na tozo hizo
kutoendana na biashara wanazozifanya.
Wameyasema
hayo wakati wakizungunza na Mpanda Radio na kusema kuwa tozo hizo ni kubwa
kwani wengi wao hawazalishi taka nyingi ambazo zinaendana na malipo hayo huku
wakidai kuwa usafi wa stendi hiyo hauridhishi.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa mtaa wa mji wa zamani bi Magreth amefafanu kuwa ulipwaji wa
tozo hizo ni wa viwango ambavyo
vimepangwa kulingana na biashara
wanazozifanya.
Usafi wa
mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu kuendelea kutunza mazingira katika hali
ya usafi ili kuzuia magonjwa ya mlipuko
yanayo sababishwa na uchafu.
No comments:
Post a Comment