Wakazi
wa mtaa wa Tambukareli katika
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameiomba serikali
kuondoa takataka katika dampo kwa wakati ili kupunguza kero wanazozipata.
Wakizungumza
na Mpanda Redio kwa nyakati tofauti tofauti wamesema kucheleweshwa kuondolewa
kwa taka hizo kumesababisha mgogoro baina ya wananchi na viongozi wa eneo hilo.
Hata
hivyo wananchi hao wamesema wamechangia fedha elfu 2000 kwa kila mtu ili kuweza kuleta gari la
kuondolea uchafu lakini mpaka sasa
uchafu bado upo na uongonzi wa mtaa huo hauja toa mrejesho wowote .
Wananchi
wameiomba serikali kuongeza magari ya
kubebea taka ili kuweza kupunguza migogoro kwa jamii .
No comments:
Post a Comment