Friday, 11 May 2018

WAKULIMA WA TUMBAKU NSIMBO. WALIA NA KUSHUKA BEI


Chama cha Msingi cha Ushirika cha Katumba Amcos  Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi kimesema changamoto za ununuzi wa zao la tumbaku kwa mwaka 2016/2017 zimesababisha kiwango cha uzalishaji wa zao hilo kupungua kwa kwaka 2017/2018.

Mwenyekiti wa chama hicho Bw.Syplian Kagoma Dioniz akizungumza na Mpanda Radio amesema,makampuni yanayonunua tumbaku yamesababisha matarajio ya kuzalisha Zaidi ya kilo laki 6 na nusu kwa mwaka 2017/2018 ukilinganisha na kiasi cha kilo Zaidi ya milioni 1.19 zilizokuwa zikizalishwa mwaka 2016/2017.

Aidha Bw.Dioniz amesema mpaka sasa kampuni ya TLTC imejiondoa katika ununuzi wa tumbaku huku kampuni ya Premium nayo ikitajwa kupunguza kiasi cha tumbaku inachohitaji kununua kwa mwaka huu.

Chama cha Katumba Amcos kina jumla ya wakulima 780 kwa sasa wakipungua kutoka 1200 kwa mwaka 2016/2017 ambapo mwaka huu bei ya kilo moja ya tumbaku inatarajiwa kununuliwa kwa dola1.75 ikipungua kutoka dola mbili kwa msimu wa kilimo uliopita 2016/2017.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...