Wananchi
kata ya kakese Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba
serikali kuwarekebishia barabara ya Misughumilo kwenda Kakese kutokana na umuhimu
wa barabara hiyo katika usafirishaji wa
mazao.
Wameyasema
hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio na kusema kuwa pamoja na barabara hiyo
kuingizia kipato kikubwa serikali lakini mpaka sasa haijafanyiwa marekebisho.
Naye
Diwani wa kata ya Kakese Maganga Salaganda amewataka wananchi wake kuwa na
subira katika kipindi hiki ambacho wanasubiria ukarabati wa barabara hiyo.
Kwa upande
wake Meneja wa Mamlaka ya Barabara mijini na vijijini Tarura Albart Kyando
amesema kuwa mpango mkakati wa kufanyia marekebisho barabara hiyo utaanza mwezi
julai kutokana na bajeti ya fedha 2018/2019.
Miundo
mbinu mibovu ya barabara imekuwa chanzo cha
kukwamisha maendeleo ya baadhi ya
maeneo hasa vijijini.
No comments:
Post a Comment