Wafanyabiashara
wa zao la mihogo na viazi katika soko la Mpanda hotel wamesema zao la mihogo liko juu ikilinganishwa
na mwaka jana katika wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Wakizungumza na Mpanda Redio kwa nyakati tofauti
wafanyabiashara hao wamesema kuwa zao hilo halipatikani kutokana na mvua nyingi
zilizonyesha mwaka huu na kusababisha
zao hilo kuharibika shambani.
Hata hivyo
wamesema kuwa zao la viazi linapatikana kwa wingi ambapo bei ya gunia kwa mwaka
huu ni sh.elf 15 na mwaka jana ilikua ni sh. elf 20
Aidha
wameomba serikari kupunguza ushuru katika mazao hayo ili wananchi waweze kunufaika na biashara
hiyo.
No comments:
Post a Comment