Zaidi ya
sh mil 26 zimechangwa na wadau
mbalimbali katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha watoto yatima kilichopo Nsemrwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Katika
harambee hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa idara ya maji katika manispaa ya
Mpanda ambapo mgeni rasmi alikuwa ni waziri mstaafu wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania Mizengo Pinda amewataka wananchi na jamii kwa ujumla kuwa na moyo wa
kujali watu wenye shida kama yatima na wajane.
Aidha
ameiomba jamii kushirikiana na madhehebu ya dini katika kusaidia na kulea
watoto yatima na ambao wanaishi katika mazingira magumu kwani ni wajibu wa kila
mtu.
Kwa upande
wa mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Raphael Muhuga amewashukuru wananchi na
jamii kwa ujumla ambao wametambua umuhimu wa kuwajali na kuwatunza watu
wanaohitaji msaada kutoka kwao.
No comments:
Post a Comment