Mpango wa
kunusuru kaya maskini TASAF Umetajwa kuwalenga zaidi walionufaika ili kupisha
walengwa wapya kupata nafasi katika mfumo huo.
Hayo
yamesemwa na Mratibu wa Tasaf Halmashauri ya Manispa ya Mpanda mkoani
Katavi Joshua Sankala kuwa walengwa
wataondolewa katika mpango kutokana na
sifa walizokuwa nazo na ndizo zitakazo waondoa huku akielezea umuhimu wa mikopo
katika vikundi.
Kwa upande
wa walengwa wa mpango huo wamesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuendelea
kuwasaidia kwani wamefanikiwa kubadili maisha yao kwa kuboresha makazi na
kufanya shughuli za ufugaji.
Mpango wa
kunusuru kaya maskini ni mpango ulioanzishwa kwa lengo la kuwasaidia wananchi
wenye hali ya chini kujikwamua kiuchumi
na ulianzishwa mwaka 2014.
Chanzo:Furaha
Kimondo
No comments:
Post a Comment