Baadhi ya Wakazi
wa kata ya Kawajense namba moja wameilalamikia serikali ya mtaa huo kutokana na kushindwa kuwapa maeneo
mapya kwaajili ya ujenzi baada ya kupisha maeneo yao ya awali.
Wakizungumza na Mpanda
Redio wamesema suala hilo limeingia dosari kutokana na kuto kuwemo katika orodha ya watu wanaotakiwa kupata viwanja
hivyo .
Hata hivyo Mwenyekiti wa
mtaa wa Kilimahewa Crispin Wasuma
amewataka wakazi wa mtaa huo kuwa na subira wakati suala hilo
likishughurikiwa ili kupatiwa ufumbuzi.
Maeneo mengi ya mkoani
Katavi yapo katika migogoro ya ardhi na mamlaka za serikali jambo linalotajwa
kuwa kikwazo cha maendeleo ya Jamii na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment