Wananchi
katika Halmashauli ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamesema,miradi
mbalimbali ambayo imezinduliwa katika manispaa ni chachu kwa maendeleo.
Wananchi
hao wametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti,wakati wakizungumza na Mpanda Radio
kuhusu miradi ambayo imezinduliwa na mwenge wa uhuru katika Halmashauri
manispaa ya Mpanda.
Aidha
wameshauri wananchi na viongozi wote kushirikiana kwa pamoja kutunza na
kuendeleza miradi kwa manufaa ya taifa.
Jumla ya
Miradi 10 ya maendeleo
yenye thamani ya shilingi milioni 800 imezinduliwa jana ambapo miongoni
mwa miradi hiyo ni pamoja na Zahanati ya Milala,Kisima cha maji,madarasa
,mabweni na barabara ya kilomita moja ya
kiwango cha lami.
Baada ya
mwenge kumaliza mbio zake katika Manispaa ya Mpanda leo umekabidhiwa Wilayani
Mlele ambapo kauli mbiu kwa mwaka 2018 ni Elimu ni ufunguo wa maisha wekeza
sasa kwa maendeleo ya taifa.
Chanzo:John John
No comments:
Post a Comment