Mwenyekiti wa
shirikisho la wafanyakazi Mkoa wa
katavi
(TUKTA) Charlse Sichilima amesema suala la watumishi kutoongezwa
mishahara lina wanavunjika moyo wa kufanya kazi kutokana na kuongezeka kwa
gharama za maisha kwa sasa .
Akizungumza na
Mpanda radio mwenyekiti huyo amesema
ongezeko la mishahara kwa wafanya kazi ni makubaliano kati ya wafanyakazi na
serikali kupitia shirikisho la wafanyakazi (Tukta) Hivyo Kitendo Cha Serikali
Kutoongeza Mishahara Kutashusha Ufanisi Wa Kazi
Aidha amesema
kuwa uwiano wa mishahara kima cha juu ni million tatu ambapo kima cha chini ni
laki tatu hivyo wanaiomba serikali kuweka uwiano sawa kwa
kiwango cha mshahara.
Mnamo tarehe 1
mwezi huu Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuri
akiwa ziarani Iringa katika kilele cha
maazimisho ya siku ya wafanyakazi amesema kuwa hatoongeza kiwango cha mishahara
kwa wafanyakazi kutokana na serikali kuwa na miradi mikubwa ya maendeleo inayo
gharimu fedha nyingi.
Chanzo:Elizabeth Jackson
No comments:
Post a Comment