Friday, 2 June 2017

Bangi yazua Kizaazaa Bungeni

Leo wakati mkutano wa saba , kikao cha 40 kikiendela bungeni Dodoma umeibuka mjadala wa dawa za kulevya aina bangi baada ya Mbunge wa Bukoba Mjini wilfred Lwakatare kuuliza swali kama moshi wa Bangi una madhara kwa ambao havuti bangi.
akijibu swali hilo naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto Hamisi Kigwangala amesema kuwa Moshi Humo umsababisha madhara sawa na yale ya Mtu anayevuta bangi.
ndipo baada ya baadhi ya wabunge wakasema kuna vitendo vinavyofanywa na baadhi ya polisi nchini vinatokana na polisi hao kuwa wamelewa bangi kutokana na kushiriki katika uteketezaji wa bangi hiyo.
Katika mjadala huo Mh Spika Job Ndugai naye alichomekea kuwa huwa anasikia watu wanasema bangi zinaongeza nguvu, hivyo naye alitaka kujua hizo bangi zinaongeza nguvu za aina gani, huki akiwauliza wabunge ambao wanatokea maeneo ambayo bangi imekuwa ikiripotiwa sana.
Kufuatia mjadala huo kuendelea alisimama Mbunge Esther Matiko Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara na kusema yeye mwenyewe huwa anaona polisi wakichoma bangi katika maeneo hayo na kudai huenda baadhi ya vitendo vinavyofanywa na polisi wetu ni kutokana na kuathirika na moshi wa bangi wakiwa wanachoma bangi hizo. Lakini katika ufafanuzi wa Naibu Waziri wa Afya alisema polisi hao wao huwa hawaathiriki na moshi huo.
 
"Jamani tunapojadili juu ya suala la madawa ya kulevya si jambo la mdhaa, ni kwamba polisi wanapokwenda kuchoma bangi mashambani huwa wanajifunika vifaa maalum lakini hata kama hawajifuniki vifaa hivyo bado ile bangi ikiingia kwenye miili yao itaondoka ndani ya siku 30 kwani inageuka na kuwa chumvi na kutoka kwa njia ya mkojo na jasho. Lakini kwa watu ambao wanatumia kila siku yaani leo, kesho, kesho kutwa na kuendelea wao wanakuwa ni clonic wa dawa hizo" alisema Kigwangalla
Licha ya Naibu Waziri wa Afya kutoa ufafanuzi juu ya uchomaji wa bangi lakini Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Joakim Mhagama alisimama na kutoa ufafanuzi wake pia akisema kuwa polisi hawajaathirika na bangi kutokana na namna ambavyo huwa wanachoma bangi hizo kwa kufuata utaratibu mzuri.
"Mh. Spika vikosi vya polisi vinavyofanya utekeketezaji wa bangi, zipo njia nyingi wanatumia kuteketeza bangi hizo, kwanza wakiwa wanafanya zoezi hilo huwa wanaangalia uelekeo wa upepo lakini pia maandalizi mengine ya vifaa vyao vya uteketezaji wa bangi, aina ya mafuta yanayotumia kwenye kuchomea bangi hizo vinawafanya kuwa salama kabisa, kwa hiyo siyo kweli kwamba likitokea tatizo kwenye jeshi la polisi kwamba polisi wetu wameathirika na matumizi ya bangi, kwani polisi wetu ni weledi na wanafanya kazi kwa kufuata utaratibu na sheria" alisisitiza Mhagama 
Kwa kumalizia mjadala huo Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kuwa nchi nzima na viongozi wamesikia juu ya jambo hilo hivyo wanapaswa kuwa makini katika utekelezaji wa mambo hayo. 

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...