Ameyasema hayo leo (Jumatatu) wakati akipokea ripoti ya pili ya mchanga wa madini uliopo katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini.
“Haya mambo yanatia uchungu, lakini kabla sijasahau ninawapongeza kamati, na ninafahamu mmefanya kazi ngumu kwa niaba ya Watanzania, ninafahamu shida mlizozipata, wengine walitaka kuhatarisha maisha yenu,” amesema.
“Nimesoma katika ripoti hii kuwa kampuni hii inafanya biashara nchini kinyume cha sheria, haijasajiliwa, hata brela haiitambui. Tujiulize sisi viongozi, dhamana tuliyopewa kuwatumikia Watanzania wenzetu tunawatumikia?” ameongeza.
“Hata shetani anatushangaa kwanini sisi ni maskini lakini tuna utajiri wa kutosha, shetani huyo huyo anawatumia Watanzania wenzetu kusababisha tuwe maskini zaidi,” amesema.
No comments:
Post a Comment