Profesa Osoro ametoa kauli hiyo leo Jumatatu alipokuwa akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo Ikulu jijini Dar es Slaam. Kamati hiyo inawasilisha ripoti hiyo ikiwa siku 18 zimepita tangu Rais apokee ripoti ya kwanza iliyoeleza kwamba, Taifa linaibiwa kupitia usafirishaji wa mchanga huo.
Baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Magufuli alitengua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na kuvunja bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) na kumsimamisha kazi mkurugenzi wa bodi hiyo.
Kamati inayowasilisha taarifa yake leo iliteuliwa na Rais na ilipewa hadidu mbalimbali ikiwamo kufanya tathmini ya usafirishaji wa mchanga huo iwapo ulizingatia mikataba ya MDAs, kuangalia kama maslahi ya Taifa yalizingatiwa, kubaini idadi ya makontena yaliyosafirishwa tangu mwaka 1998.
"Matokeo ya uchunguzi huu yanaonyesha kuwa kampuni ya Acacia haina sifa za kuchimba wala kufanya biashara ya madini hapa nchini, inafanya shughuli zake kinyume cha sheria za nchi, hii inashangaza sana,"alisema.
mapendekezo
1.serikali ichukue hatua za kisheria dhidi ya Acacia2.serikali idai kodi.
3.serikali iendelee kuzuia hadi kodi ilipwe
4.serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria kwa mawazari, wanasheria na watu wote waliohusika kuliingizia taifa hasara
5.serikali ifute utaratibu wa kupokea utaratibu wa asilimia 90 ya mraaba na asilimia 10 baadae.
6.uchunguzi kuhusu mwenendo wa watumishi wa idara ya walipa kodi wakuba TRA
7.Banki kuu ifatilie mauzo ya kigeni.
9.sheria iongeze kiwango cha adhabu ilianishwa kwa wakwepaji wa kodi.
10. kuondoa misamaha yote isiyokuwa na tija kwa taifa.
11. kiwango cha hisa za serikali kiwe maaalum
12. udhibiti wa biashara haramu kwa uanzishwaji wa kitengo maalum.
13 mikataba isiwe ya siri na iridhiwe na bunge kabla ya utekelezaji.
14. sheria ioneshe mchanganuo wa kina wa uendeshaji.
15 kuondoa masharti yasiyo kuwa na manufaakwenye mikataba.
16. kupita kamishina wa madini kufanyike ukaguzi wa marakwa mara wa uendeshaji
No comments:
Post a Comment