Na, Alinanuswe Edward
DIWANI wa Kata ya Mwamkuru iliyopo halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Kalpi Katani amewataka wakulima na wakazi wa eneo hilo kuaachana na uuzaji wa mazao ya chakula Kiholela.
DIWANI wa Kata ya Mwamkuru iliyopo halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Kalpi Katani amewataka wakulima na wakazi wa eneo hilo kuaachana na uuzaji wa mazao ya chakula Kiholela.
Zao la Mpunga |
Amesema kuwa katika msimu huu wa mavuno imebainika
kuwepo kwa walanguzi wanao walaghai wakulima na kununua mazao kwa bei ya chini
jambo ambalo halimnufaishi mkulima na kwamba hawatolifumbia macho suala hilo.
"Walanguzi wa mazao wamekuwa wakiwashawishi wakulima kuuza mazo yao, kwa bei ambayo ni ndogo na haimletei faida huyu mkulima, tuna mpango wa kuhakikisha tunapambana nao ili huyu mkulima anufaike na mazao yake" alisema Katani.
Katika hatua nyingine diwani huyo amesema wakulima wawe
makini katika kipindi hiki hasa kwa kukumbuka kuweka akiba ya chakula.
Kata ya Mwamkuru ni maarufu kwa uzalishaji wa zao la mpunga
hasa kutokana na uwepo wa kilimo cha umwagiliaji katika eneo hilo.
Katika juhudi za kukabiliana na njaa Mwezi March 2017 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali mstaafu
Raphael Muhuga aliamuru idara mbali mbali zinazo husika na masuala ya kilimo,
biashara na Kijamii kuhamasisha jamii kuweka akiba ya chakula.
Mwaka 2016 mwishoni suala la uwepo wa njaa nchini au laa
liliibua mjadala mkubwa kutoka kwa wanasiasa na baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia vyama pinzani kumtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli atangaze janga la njaa jambo ambalo
alilipinga vikali na kutaka wananchi wachape kazi.
No comments:
Post a Comment