Monday, 24 July 2017

RAIS WA POLAND APINGA MISWADA TATA ILIYOPITISHWA BUNGENI

Rais wa Poland Andrzej Duda ametumia kura yake ya turufu kupinga miswada miwili kati ya mitatu inayoufanyia mageuzi mfumo wa idara ya mahakama nchini humo.

 Hatua hiyo inatuliza hofu kuwa chama tawala cha Sheria na Haki kitahujumu mgawanyo wa madaraka.

 Duda amesema ataurudisha bungeni mswada kuhusu Mahakama ya Juu pamoja na ule unaohusu Baraza la Kitaifa la Mahakama.

Kumekuwa na maandamano nchini Poland tangu miswada hiyo ilipopitishwa na mabunge yote mawili. Wakosoaji walisema sheria hizo zingeathiri uhuru wa mahakama kwa kuwapa wanasiasa nguvu za kuwaajiri na kuwafuta maafisa wa mahakama.

 Aidha, wachambuzi wanasema uamuzi wa Duda unamweka katika mgongano na kiongozi halisia wa nchi hiyo ambaye ni kiongozi wa chama tawala cha PiS lakini hana wadhifa rasmi serikalini.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...