Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na mkewe bi Grace Mugabe
|
Maafisa
wa polisi wa Afrika Kusini wametoa tahadhari dhidi ya Mkewe rais Mugabe katika
mipaka ya taifa hilo , waziri wa polisi nchini humo amesema.
Ametuhumiwa
kwa kumpiga na kumjeruhi mwanamke wa miaka 20 katika kichwa chake katika chumba
cha hoteli karibu na mji wa Johannesburg .
Polisi
wanatariaji kwamba Bi Mugabe mwenye umri wa miaka 52 alipaswa kujiwasilisha
mbele yao siku ya Jumanne lakini akakataa kufanya hivyo.
Bi Grace
mugabe kwa sasa hajulikani yu wapi lakini inaaminikwamba bado yupo Afrika
Kusini.
Rais wa
Zimbabwe Robert Mugabe pia amewasili nchini Afrika Kusini kwa kikao cha
viongozi wa mataifa ya Afrika Kusini SADC kinachoanza kuanza leo siku ya Ijumaa.
Bi Mugabe
hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.
Waziri wa polisi Fikile Mbalula alisema: Sisi polisi
wa Afrika Kusini tayari tumeweka notisi katika mipaka yetu yote ili kumzuia bi
Mugabe kuondoka nchini siku ya Jumatano, wakili wa Afrika Kusini Gerrie Nel
aliyefanikiwa kumshtaki mwanariadha mlemavu Oscar PIstorius
Pia limesema
kuwa litakabiliana na hatua yoyote ya kumpatia kinga ya kidiplomasia bi Mugabe.
Bi Engels
alisema kwamba alishambuliwa na bi Mugabe aliyeamini kwamba alikuwa akijua kule
aliko mwanawe Bellarmine.
''Tuliendelea kumwambia hatujui
aliko...hatujamuona usiku wote...alinikamata na kuanza kunipiga.Nakumbuka
nikianguka katika sakafu na damu nyingi katika uso na shingo yangu.Alitupiga
akiwa na chuki nyingi'', alisema msichana huyo.
habari kutoka bbc.
No comments:
Post a Comment