Thursday, 10 August 2017

BILLIONEA BILL GATES ASHIKILIA SEKTA YA KILIMO NA AFYA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli akizungumza na Billionea Bill Gates Ikulu jijini Dar Es Salaam






DAR ES SALAAM 

Rais John Pombe Magufuli amemshukuru Mwenyekiti Mwenza wa taasisi ya Bill and Mellinda Gates Bw. Bill Gates kwa misaada mbalimbali ambayo inatolewa kupitia taasisi yake kwenye miradi mbalimbali nchini. 


Rais Magufuli amesema hayo leo alipokutana na tajiri huyo Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo waliweza kufanya mazungumzo mbalimbali na kampuni hiyo kusema imetenga Dola za Marekani Milioni 350 sawa na takribani Shilingi Bilioni 777.084 za Tanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali katika sekta ya kilimo, afya na mifumo ya kielektroniki ya upatikanaji wa taarifa.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Bw. Bill Gates kwa mchango mkubwa unaotolewa na taasisi ya Bill and Mellinda Gates katika miradi mbalimbali hapa nchini ikiwemo fedha ambazo taasisi hiyo itazitoa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia sasa na amemhakikishia kuwa Serikali yake itahakikisha fedha hizo zinaleta matokeo yaliyokusudiwa.

Mazungumzo kati ya Mhe. Rais Magufuli na Bw. Bill Gates yamehudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Ufugaji na uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu




No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...