Taarifa kutoka Uganda zinaeleza
kwamba Watanzania 13 waliokuwa kwenye basi hilo wamefariki na wengine wanane
kujeruhiwa vibaya baada ya basi hilo kugongwa na lori.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi amethibitisha taarifa ya ajali ya gari
iliyotokea Uganda na kuhusisha basi aina ya Costa lenye namba za Tanzania na
lori la Uganda ambalo lilikuwa limetokea Dar es Salaam.
Taarifa kutoka Uganda
zinaeleza kwamba Watanzania 13 waliokuwa kwenye basi hilo wamefariki na wengine
wanane kujeruhiwa vibaya baada ya basi hilo kugongwa na lori.
Kamanda
Ollomi amesema Watanzania hao walikwenda Uganda kwa ajili ya shughuli ya harusi
lakini hana taarifa walikwenda sehemu gani nchini humo. Amesema wanaendelea
kufanya mawasiliano na mamlaka za Uganda kujua undani wa ajali hiyo.
“Ni kweli
tumefuatilia basi hilo na kubaini kwamba liliondoka hapa nchini Septemba 15
kwenda Uganda kwenye shughuli ya harusi. Mengine siwezi kusema zaidi mpaka
tutakapofanya mawasiliano na mamlaka za Uganda,” amesema Ollomi.
Gazeti la Uganda la Daily Monitor limeandika mtandaoni kwamba
Watanzania hao walikwenda Uganda kwenye harusi ya binti yao, Dk Annette
Ibingira ambaye amefunga ndoa na Mganda, Dk Treasurer Ibingira.
No comments:
Post a Comment