Maelfu ya abiria walikwama kwenye uwanja wa ndege wa Auckland nchini New Zealand leo Jumatatu, baada ya bomba la mafuta kupasuka na kusababisha uhaba wa mafuta ya ndege kwenye uwanja wa ndege.
Bomba lililopasuka ndilo peke yake linalopeleka mafuta uwanjani humo.
Tatizo hilo linatarajiwa kudumu wiki moja wakati jitihada zinafanyika kulikarabati bomba hilo
Kumekuwa na ugavi wa mafuta na mashirika mengi ya ndege huongeza ndege zao mafuta nchini Australia na sehemu zingine kwa ndege zinazosafirisha miendo mirefu.
Kulingana uwanja wa ndege wa Aukland unaowahudumia wateja milioni 18 kila mwaka, ni kuwa kampunii za mafuta ndiyo uhusika na usafirishaji wa mafuta yanayotumiwa na ndege na kuwa uwepo wa mafuta hayo umeshuka.
Shirika la Air New Zealand linasema kuwa abiria 2000 walioathiriwa na kufutwa kwa safari leo Jumatatu.
Sawa na Air New Zealand mashirika ya Qantas, Cathay Pacific na Emirates yamesema kuwa badhi ya safari zimeathiriwa na uhaba huo wa mafuta.
Takriban safari 27 za kigeni na za ndani ya nchi zilifutwa mwishoni mwa wiki hii nchini New Zealand.
@habari na bbc swahili
No comments:
Post a Comment