Monday, 18 September 2017

Wananchi wanatakiwa kushiriliana na jeshi la kuripoti kwa wakati matukio mbalimbali ya kiuharifu yanayoendelea kutokea wilayani Mpanda.

MPANDA
JESHI la polisi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi limewataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo kuripoti kwa wakati matukio mbalimbali ya kiuharifu yanayoendelea kutokea wilayani Mpanda.
Wito huo umetolewa na kaimu mkuu wa Kituo cha Polisi Wilayani Mpanda Insepcta Stephen Kisaka ambaye pia ni Mkaguzi wa Polisi katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika mtaa wa Mpadeco kata ya Makanyagio.

Aidha Inspecta Kisaka ambaye pia ni mlezi wa kata ya Makanyagio amewatoa hofu wananchi  kuwa siri za kiuharifu watakazozitoa zitahifadhiwa kwa kuwa jeshi la polisi kwa sasa kwa lengo ni kutokomeza uharifu.

Naye Mwenyekiti wa mtaa wa Mpadeco Bw.Benard Nkana ameagiza wenye nyumba wote katika mtaa huo kutopangisha watu au wageni katika nyumba zao bila kutoa taarifa kwa viongozi kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mwenye nyumba.

Source Issack Gerald

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...