Monday, 18 September 2017

WAKAZI wa Mtaa wa Mpadeco wamemlalamikia diwani wa kata hiyo kutofanya mikutano kusikiliza kero tangu alipochaguliwa mwaka 2015.

MPANDA

WAKAZI wa Mtaa wa Mpadeco Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamemlalamikia diwani wa kata hiyo  kutofanya mikutano kusikiliza kero  tangu alipochaguliwa mwaka 2015.
Wakizungumza katika  mkutano wa hadhara uliofanyika  katika mtaa huo wamesema hawaoni uboreshwaji wa miundo mbinu na masuala mengine ya kijamii yakifanywa kama alivyo ahidi .

Kwa upande wake diwani wa kata ya Makanyagio Hidary Sumry amekili kutofanya mikutano katika eneo hilo kwa madai kuwa mikutano inaendeshwa kwa mipango ikiwemo gharama.

Mtaa wa Mpadeco wenye una zaidi ya wakazi elfu moja lakini hauna vizimba vya kutupa taka hali ambayo wakazi wa eneo hilo wanadai kuwa ni uzembe wa viongozi.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...