Wafanyakazi wa mpanda radio wakiwa na askari ya jeshi la zimamoto |
KATAVI.
Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani
Katavi limesema linaanza oparesheni ya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba ili kubaini watu wenye tabia ya kuchimba vyoo
au visima na kuacha bila kufukia mashimo
hayo hali ambayo husababisha vifo vya
watu .
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa
Ukaguzi wa Jeshi la Zima moto Kopro
Wilfred Ruhega wakati akizungumza na mpanda redio na kusema kuwa ambaye
atabainika anashindwa kutii sheria bila shurti hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yake.
Mkuu wa Ukaguzi
Ameongeza kuwa zoezi hilo la ukaguzi
unaofanywa kwenye majengo pamoja na vyombo vya usafiri unaenda sambamba na tozo
ambazo zipo tofauti kulingana na eneo husika.
Kwa upande wake Kopro Pastori Stanslaus Skwara Mthamini wa jeshi hilo mkoani katavi amesema viwango tofautitofauti vilivyoainishwa vimepangwa kwa mujibu wa sheria hivyo ni vema wananchi kutii sheria bila shurti.
Kwa upande
wa Afisa Rasilimali watu Koplo Lazaro
Nditya amesema kuwa watafika eneo la
tukio ikiwa taarifa imetolewa kwa wakati kutokana na kuwepo kwa askari masaa
ishirini na nne na kuwaasa wananchi kuachana kupiga cm bila kuwa na shida
yoyote hai ambayo hupelekea kuleta usumbufu.
No comments:
Post a Comment