Dodoma.
Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza biashara ya madini ya
almasi imependekeza wajumbe wote wa bodi na waliohusika na kusimamia mgodi wa
madini hayo, wahojiwe na ikibainika wamehusika mapungufu wachukuliwe hatua.
Akisoma ripoti ya kamati hiyo ambayo itakabidhiwa kwa Spika
wa Bunge Job Ndugai ambaye ataikabidhi kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
mwenyekiti wa kamati hiyo, Mussa Zungu amesema wamebaini madudu mengi.
Madudu hayo ni pamoja na upotevu wa kodi, kutosimamiwa vyema
kwa uchimbaji wa madini hayo, tofauti kubwa kati ya takwimu zinazotolewa na
taasisi za Serikali juu ya kiasi kilichopatikana na kuuzwa cha madini hayo na
udanganyifu kuhusu hali na gharama za mitambo.
"Serikali ihoji wajumbe wa bodi na wote ya migodi hii
na wote wanaohusika na ikibainika kuwa walihusika katika mapungufu waliyoyaona
wachukuliwe hatua,"alisema.
@habari toka mwananchii
No comments:
Post a Comment