MPANDA.
Waendesha pikipiki za
matairi matatu maarufu kama bajaji katika manispaa ya Mpanda wameomba kuongezwa
kwa maeneo mapya ya maegesho kwa ajiri ya shughuri hiyo.
Wakizungumza na Mpanda
radio fm baadhi ya waendsha Bajaji hao katika maegesho ya soko kuu lilipo katikati
ya mji wa Mpanda wamesema kumekuwa na ongezeko la bajaji kila uchao lakini
mamlaka hazichukui hatua zozote hali inayopelekea kuongezeka kwa msongamano na kuhatarisha usalama .
Katika hatua nyingine
wamewatuhumu viongozi wa umoja wa waendesha bajaji kwa kujipatia fedha kwa njia
zisizo halali kutokana na kukosekana kwa udhibiti wa mamlaka zingine.
Kwa upande wa mhasibu
wa umoja wa waendesha bajaji aliyejitambulisha kwa jina moja la BW Komba
amekanusha suala hilo na kufafanua kuwa fedha zinazokusanywa hutumika kwa
mujibu wa makubaliano yao.
No comments:
Post a Comment