MPANDA
Wananchi Mkoani katavi
na Tanzania kwa ujumla wameombwa kutumia fursa za ujasiriamali ili kujikwamua
kiuchumi na kuleta maendeleleo katika familia zao.
Mkurugenzi wa mafunzo ya ujasiriamali kutoka Kampuni ya VIEN Bw. Mabiru Almasi katika mafunzo ya ujasiliamali
yanayoendelea kutolewa katika ukumbi wa kanisa la Roman Katoliki yaliyoandaliwa
na Mpanda Redio kwa kushirikiana na kampuni hiyo.
Aidha amesema ni wakati
wa watu kujiingiza katika ujasiriamali badala ya kusubiri kuajiriwa maana fursa
ni nyingi kama watu watajishughulisha na kujituma katika kazi za mikono yao.
Kwa upande wa washiriki
wa semina hiyo wamesema wamejifunza mambo ambayo yatawasaidia kujikwamua
kiuchumi na kuweza kuongeza kipato ambacho kitawasaidia katika familia zao.
Semina ya ujasiliamali
imeanza jana na inatarajia kumalizika kesho jioni huku ikiwa imewanufaisha
wananchi wengi ambao wamehudhuria kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi na
nje ya Mkoa wa Katavi.
@habari na Rebeca
Kija.
No comments:
Post a Comment