Muhingo Rweyemamu enzi za uhai wake |
Muhingo Rweyemamu aliongoza halmashauri za
Handeni, Makete na Morogoro akiwa mkuu wa wilaya.
Baada
ya kikao cha mashauriano, imekubaliwa mwanahabari mkongwe na Mkuu wa Wilaya
mstaafu, Muhingo Rweyemamu atazikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es
Salaam.
Taarifa iliyotolewa na familia imesema maziko
yatafanyika Jumanne, Septemba 5.
Kabla ya maziko imeelezwa kutakuwa na ibada ya
kuaga mwili wa Muhingo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
Mbezi, Kibanda cha Mkaa.
Familia imesema mwili wa marehemu unatarajiwa
kufikishwa nyumbani kwake Mbezi Luis kesho Septemba 4, ambako utalala.
Muhingo (67), alifariki dunia jana Septemba 2,
katika Hospitali ya Aga Khan jijini hapa.
Kabla ya Rais Jakaya Kikwete wa Serikali ya
Awamu ya Nne kumteua Muhingo kuwa mkuu wa wilaya, alikuwa akifanya kazi za
uandishi wa habari.
Mtoto wa marehemu, Mwesigwa Muhingo amesema kifo
cha baba yake kimetokana na maradhi yaMyelofibrosis yanayotokana na mifupa
kushindwa kutengeneza damu.
No comments:
Post a Comment