Mtandao
wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikaina na Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi imeanza kuhamasisha wanawake wenye kipato cha chini
kumiliki ardhi iliyopimwa ili wakopesheke na kuboresha biashara zao.
Mkurungenzi wa TGNP, Lilian Liundi alisema jana
kuwa lengo ni kuwezesha wanawake wenye kipato kidogo kupata mikopo.
Pia, TGNP inazungumza na benki za biashara
kuwapatia mikopo wanawake wenye viwanja vilivyopimwa, ili kukopeshwa kwa riba
nafuu na kujikwamua na umaskini.
“Miaka iliyopita Tanzania imepiga hatua kwenye
mambo ya usawa na jinsia, lakini changomoto ni upatikanaji na umiliki wa ardhi
iliyopimwa kwa wanawake,” alisema Liundi.
Alisema ushiriki mdogo wa wanawake katika ngazi
za uamuzi, unyanyasaji wa jinsia na kuwashirikisha kwenye mambo ya uchumi bado
ni changamoto. Naye Ofisa Habari wa TGNP, Deogratius Temba alisema taasisi
binafsi na umma zinatakiwa kushirikiana ili kuhakikisha wanawake
wanashirikishwa kwenye uchumi kwa maendeleo ya Taifa.
No comments:
Post a Comment