Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amemteua Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.
Taarifa iliyotolewa
na Ikulu imesema uteuzi huo unaanza leo Jumapili.
Kabla ya uteuzi huo,
Profesa Juma alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Januari alipostaafu Jaji Mkuu,
Mohamed Chande Othman.
Ikulu imesema Jaji
Mkuu ataapishwa kesho Jumatatu saa nne asubuhi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli Januari
17 alimteua Profesa Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu.
Kabla ya kuteuliwa
katika nafasi hiyo, Profesa Juma alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa.
Jaji Mkuu mstaafu
Chande hadi kufikia Januari Mosi alikuwa ameshafikisha miaka 65 ambayo ni ya
kustaafu majaji wa Mahakama ya Rufani kama ilivyobainishwa katika Ibara ya 120
ya Katiba ya mwaka 1977.
Jaji Chande
aliteuliwa katika nafasi hiyo na Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2010
akichukua nafasi ya Jaji mstaafu Augustino Ramadhani.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, uteuzi huo unaanza Jumapili ( Septemba 10, 2017).
Kabla ya Uteuzi huo Profesa Ibrahim Hamis Juma alikuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania ambapo alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.
Taarifa hiyo ya Ikulu inasema Profesa Ibrahim Hamis Juma ataapishwa kesho Septemba 10, 2017 saa nne asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment