Thursday, 7 September 2017

Serikali imetenga shilingi milioni Bilioni 500 Kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha afya katika Kata ya Majalila.

Mbunge wa wilaya Tanganyika Mhsulemani kakoso

TANGANYIKA
Serikali imetenga shilingi milioni Bilioni 500 Kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha afya katika Kata ya Majalila ambayo ni makao makuu ya wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi.

Hayo yamesemwa na leo bungeni Dodoma na Naibu wazili wa ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Tamisemi Mh Seleman Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Mpanda vijiojini Suleiman Kakoso aliyetaka kujua mkakati wa serikali wa kujenga kituo cha afya katika wilaya hiyo.

Katika majibu yake amemhakikishia mbunge huyo kuwa tayari mipango yote imefanywa  kinachosubiliwa ni utekelezaji wa kuanza kwa ujenzi wa majengo katika eneo hilo.


Wilaya ya Tanganyika imetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake makao yake makuu ni kijiji cha majalila.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...