Rais wa tanzania Dk John Pombe Magufuli |
Ripoti hizo zimetokana na kamati
mbili zilizoundwa na spika wa Bunge Job Ndugai. Mara baada ya kupokea ripoti
hizo, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa wateule wote waliotajwa katika ripoti
hizo.
Miongoni mwa wateule wa Rais
waliotajwa katika ripoti hiyo ni pamoja na Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI,
George Simbachawene, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Edwin Ngonyani.
Wengine waliotajwa katika taarifa hizo ni pamoja na Katibu Tawala Eliakim
maswi, wabunge Willium Ngeeleja na Endrew Chenge.
"Kuna baadhi ya wabunge kama
ulivyosema mheshimiwa Spika, kila mahali yupo, katika kashfa fulani yupo,
katika hili yupo, katika lile yupo. Tena wengine bado wapo bungeni na wakati
mwingine wanachangia mpaka mishipa inawatoka, taratibu zifanyike kuwachukulia
hatua" Rais Magufuli Rais Magufuli amewasifu watanzania wazalendo ambao
wako tayari kutoa uhai wao kwa ajili ya Taifa lao.
"Tunawatumia watanzania
wazalendo kupata taarifa za kizalendo kwa Taifa letu, wapo watanzania
wanaorubuniwa na kuisaliti nchi yao, hao hawafai" Rais Dk John Pombe
Magufuli, Ikulu. Dar es Salaam.
Katika maelezo yake kabla ya
kumkabidhi Rais ripoti hizo, Majaliwa amesema kwa muda mrefu watanzania
wamekuwa wakilalamika serikali kutowajali na kuwasikiliza. Amesema kupitia
serikali ya Awamu ya Tano sasa watanzania wote watakuwa na haki sawa na wote
watasikilizwa.
"Watanzania ambao kwa miaka
mingi wamejihisi hawasikilizwi na hawahurumiwi sasa ni wakati wao kujihisi kuwa
ni watanzania na wanastahili haki zote kama watanzania kupitia serikali yako
mheshimiwa Rais" Kassim Majaliwa
Rais Magufuli amemkabidhi Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU kwa ripoti hizo za madini kwa ajili ya kufanyiwa kazi mara
moja.
No comments:
Post a Comment