Dodoma.
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na
kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.
Katibu
wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman
Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali
hiyo kujua kinachoendelea.
Baadhi
ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya
mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Charles Kihologwe amewataka watu hao kukaa mbali na chumba cha upasuaji
lakini wengi wanakataa wakisema hawamwamini mtu yeyote.
Asubuhi,
Lissu alihudhuria kikao cha Bunge na aliomba mwongozo wa Naibu Spika akihoji
kuhusu taarifa za kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutathmini
mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na
almasi kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu badala ya kujadiliwa na Bunge kwanza
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe amesema “hali ya Tundu Lissu ni mbaya”
@Habari toka mwananchi
No comments:
Post a Comment