Mbunge viti maalumu mkoani Katavi Mh.Roda Kunchela |
Serikali
inatalajia kulipa fidia kwa wananchi kutokana na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Mpanda kuelekea
Mkoani Kigoma kwa mujibu wa sheria.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Dodoma na Naibu waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Mh.Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la mbunge viti maalumu mkoani Katavi Mh.Roda Kunchela utaratibu wa ulipaji wa fidia kwa wananchi hao.
Katika hatua hiyo Waziri Ngonyani amesema serikali inatambua suala hilo na kuwahakikishia waathiriwa wa ujenzi wa barabara hiyo malipo yao kwa wakati.
Hata
hivyo Mh.Ngonyani amesema serikali haitawalipa fidia wananchi wasiokuwa na sifa
ya kupewa fidia.
No comments:
Post a Comment