Tuesday, 19 September 2017

Wafuasi wa Kenyatta wailaumu mahakama kuwaibia ushindi

Maandamano ya wafuasi wa uhuru kenyattaHaki miliki ya picha
Image captionMaandamano ya wafuasi wa Uhuru Kenyatta wakiwa nje ya mahakama kuu mjini Nairobi
Wafuasi wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wanaandamana nje ya mahakama kuu mjini Nairobi, wakiitaka tume ya kitaifa inayoajiri na kufuatilia mienendo ya majaji iwachunguze.
Kwa mujibu wa ukurasa wa Twitter wa gazeti la kibinafsi la Daily Nation, Wafuasi wa Kenyatta wamekusanyika wakiwashutumu majaji wa mahakama kuu kwa kuwaibia "ushindi wao ".
Majaji wa mahakama hiyo walitoa uamuzi wa kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais wa tarehe 8 Agosti yaliyompatia ushindi Bwana Kenyatta baada ya kusema kuwa mchakato wake ulitawaliwa na "ukiukaji wa sheria na makosa"
Maandamano hayo yamefanyika wakati gazeti la The Standard kuchapisha taarifa ya madai kwamba majaji wawili wa Mahakama kuu , Philemona Mwilu na Isaac Lenaola, ambao walipigia kura kubatilishwa kwa uchaguzi, walikutana na mawakili wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, wakati wa kusikilizwa kwa kesi ya kupinga ushindi wa Bwana Uhuru Kenyatta.
Taarifa hiyo iliyotawala mazungumzo ya raia wa Kenya kwenye mtandao wa Twitter,pia inasema kuwa kuna mazungumzo ya simu yaliyo rekodiwa kuthibitisha kwamba kulikuwa na mawasiliano baina ya majaji na mawakili wa upinzani waketi kesi hiyo ikiendelea.
mwandishi wa habari nchini humo ameripoti kuwa waandamanaji wamekwisha wasilisha madai yao kwa tume ya huduma za mahakama inayowaajiri na kuchunguza mienendo ya majaji nchini Kenya.
@habari toka Bbc swahil

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...