MPANDA.
Baadhi
ya wakazi wa kata ya Litapunga Halmashauri
ya Nsimbo Mkoani Katavi wamelalamikia ubovu wa barabara inayotoka Mnyaki
kuelekea kijiji cha Kaburonge A na B.
Wananchi
hao akiwemo Bi. Janeti Sadi wamesema kuwa ubovu wa barabara hiyo hasa daraja
linalounganisha eneo la Mnyaki na Kaburonge inaweza kusababisha vifo kwa
wagonjwa.
Sadekia
Ndikumana Mwenyekiti wa kijiji cha Kaburonge A amesema ubovu wa barabara hasa daraja umekuwa ni wa
kipindi kirefu na wamekuwa wakimlilia
diwani juu ya suala hilo lakini hawaoni
juhudi zozote za kutatua changamoto hiyo.
Diwani
wa Kata ya Litapunga Juma Masoud Mnyongagule amesema wapo katika mchakato wa
kutatua changamoto hiyo.
Aidha
diwani Mnyongagule amewaomba wananchi kuwa na subira kwa kusema anashirikiana
na Wenyeviti wa vitongoji, Vijiji pamoja na watendaji wa kata ili kuletea taifa
maendeleo.
@habari na Mdaki Hussein.
No comments:
Post a Comment