Kizimba cha kutunzia taka |
MPANDA
WAKAZI wa kata ya Mpanda Hotel
Manispaa ya Mpanda wamelalamikia uwepo wa taka katika makazi yao kwa muda mrefu
hali inayosababisha kuhofia magonjwa ya mlipuko.
Wakizungumza na Mpanda radio wamesema
uchafu umerundikana majumbani na barabarani kwa zaidi ya wiki tatu bila
kuzolewa licha ya kila mwezi kuchanga pesa kwa ajili ya uzoaji taka.
Mwenyekiti wa kikundi cha kuzoa taka
katika Kata ya Mpanda Hotel Bw. Emmanuel Mgiuna amesema wanashindwa kuzoa taka
kwa sababu hakuna gari wala kizimba kwa ajili ya kukusanyia uchafu.
Kwa
upande wake Afisa mtendaji wa kata ya Mpanda Hotel Bw.Hamidu Sungura amekataa
kuzungumzia tatizo la mrundikano wa taka katika Kata ya Mpanda Hotel huku naye
Bibi Afya wa kata hiyo Bi.Grace Kunchela kwa sharti la kutorekodiwa sauti
akisema zoezi la kuzoa litaanza kesho
Source Mdaki Hussein
No comments:
Post a Comment