ARUSHA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunagano wa Tanzania
Kasimu Majaliwa ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji ulio
katika mji wa Longido mkoani Arusha.
Waziri mkuu amesema mradi huo utagharimu kiasi cha sh.bilioni 16 hadi
kukamilika kwake na tayari wakandarasi wanne
wameshaanza kuifanya kazi hiyo.
Aidha amewataka wananchi wa maeneo jirani na
nje ya mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa kama kuanzisha viwanda mbalimbali kutokana
na uwepo wa huduma ya maji katika mji huo.
Baadhi ya
wakazi wa wilaya ya Longido wameitaja huduma ya maji kama neema katika
eneo hilo kwa kile walicho kiita kuwa hapo awali ilikuwa kama jambo la
kufikilika tu.
Mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakazi wa eneo hilo
zaidi ya 2000 ambao utapunguza tatizo la maji kwa kiasi kikubwa katika maeneo
hayo.
@habari na Mwananchi
No comments:
Post a Comment